Header Ads

Breaking News

TSJ YAIBUKA KIDEDEA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UTANGAZAJI WA VYUO....





Haya ndio makombe yaliyoshindaniwa

Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji TSJ kibeibuka kidedea jana jioni katika mashindano ya utangazaji wa vyuo na kupata alama za juu katika vipingele nne ambavyo ni Serious Program, uchambuzi wa magazeti, Michezo pamoja na Burudani.

Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya Chuo cha Tsj maeneo ya Ilala Sharifu Shamba yalijumisha idadi ya vyuo sita
(6) lakini vyuo ambavyo vilishiriki jana katika kinyang’anyiro hicho ni vitatu (3) ambavyo ni Royal wanatokea Ubungo Urafiki,  Dacico wao wanatokea Kimara mwisho pamoja na Tsj kilichopo Ilala Sharifu Shamba.

Nafasi ya pili ya shindano hili walishika Chuo cha Royal japokuwa walikataa kuchukua kikombe cha ushindi wa pili kwasababu zilisokuwa na msingi na kuanzisha fujo katika maeneo ya mashindano hapo kwa wenyeji wao Tsj.

Wakiongee na ukurasa huu jana kundi la wanafunzi wa Tsj walisema “ sisi ndio sisi ushindi kwetu daima kwani tulijiandaa vya kutosha japokuwa mda tuliyofanya mazoezi ni mdogo mno ila tumestahiki kuwa mshindi wa nafasi ya kwanza”

Makamu wa Rais wa Tsj akibeba kombe la Mshind wa nafasi kwanza katika chuo chake
Naibu Waziri wa Shirikisho la vyuo kutoka Tsj nae akibeba Kombe la Nafasi ya kwanza
Hii ndio Serikali ya wanafunzi wa Tsj baadhi yao waliokuwepo siku hiyo.
Hii ndio Serikali ya wanafunzi wa Tsj baadhi yao waliokuwepo siku hiyo
Upande wa kushoto ni Mkuu wa chuo cha uandishi habari na utanagazji Bi Carlyina Setumbi anayafuatana nae pembeni yake ni Rais wa Tsj Bi Frida Matinya wakiambatana na Makamu wake Bw. Elly Mhagama na wa mwisho upande wa kulia huyo ni mratibu wa masomo hapoa Tsj Bi Brandina Semaganga.
Hii ni picha ya pamoja wafanyakazi wote wa Tsj Kuanzia ngazi ya juu ya Principal (Mkuu wa Chuo)
mpaka mtu wa library (Mkutubi)

No comments