ANGALIA VIDEO JINSI OMMY DIMPOZ ALIVYOPIGWA NA CHUPA JANA NA MASHABIKI WA MUZIKI WA DODOMA KUTOKANA NA SKENDO YA KUMTUKANA MAREHEMU ALBERT MANGWEA #KILI MUSIC TOUR##
Ile skendo ya Msanii Ommy Dimpoz kumtolea maneno ya kejeli na matusi
aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea imemtokea
puani mbana pua huyo mara baada ya kutinnga Dodoma katika ile Tour ya
washindi wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards na kushindwa kufanya kile
alichokusudia kukifanya......STORY INAENDELEA
Ommy Dimpoz kama kawaida yake unaweza kuamini hata hayo maneno ambayo
anayakanusha ya kumtukana Ngwea yasikuingie akilini pale ambapo
alisimama na kutoa maneno machache tu tena hata bila ya kuwa na
msisitizo wowote ama kuonesha kweli alisingiziwa. Msanii huyo aliweza
kutamka tu kifupi kwa kuwaambai mashabiki kuwa "Mimi nakiri kwamba
sikumtukana Albert Mangwea" baada ya kutoa maneno hayo alimruhusu Dj
aweze kuendelea na yake na show ikaanza.
Lakini mara tu baada ya wimbo wake wa kwanza kuisha uliofuata wa pili
alijikuta akiwa na kazi mbili yaani kuimba na kukwepa chupa zilizokuwa
zikirushwa na mashabiki ambao wote walikuwa wakimtaka aondoke haraka
jukwaani na kama sio nguvu ya ziada ya walinzi kumlinda kwa kuzuia chupa
hizo na kumshawishi ashuke haraka huenda hata angepata majeraha
asoyatarajia, ilibidi akubali matokeo kwamba mashabiki hawamtaki na
ndipo aliposhuka hukua akiwaacha madancer wake wakiendelea kuumalizia
wimbo wake kwa kucheza kwa aibu kabla nao hawajamfuata boss wao.
Tour hiyo ya Kili Music ilizinguliwa Jioni ya Jumamosi tarehe 22/06/2013
mkoani Dodoma na itafuatiwa na mkoa wa Tanga na kuendelea na mikoa
mingine.
No comments
Post a Comment