Header Ads

Breaking News

HII NDO VIDEO YA D'BANJ NA DON JAZZY WAKIIMBA PAMOJA BAADA YA KUWA NA BIFU KUBWA SIKU ZA KARIBUNI....


Wakali hawa wawili kwenye music kutoka Nigeria, D Banj na Don Jazzy ambaye ndiyo producer wa ngoma kali za D Banj kama Fall in Love na nyingine nyingi. Baada ya wote wawili kupata dili kwenye lebo ya Kanye West, ulitokea ugomvi mkubwa kati
ya washkaji hawa wakubwa bila ya chanzo kuwekwa wazi vizuri. Ugomvi huo ukiendelea zilivuja emails kwenye mtandao ambapo Don Jazzy alikuwa anamwambia D Banj arudishe magari ambayo aliyompa kipindi cha nyuma

Hivi sasa habari mpya kuhusu beef lao ni kwamba wanaelekea kupatana kwa kile kiliichonekana mbele ya watu wengi. Don Jazzy alihudhuria kwenye sherehe ya ndoa ya mdogo wake D Banj ambaye alikuwa anafunga ndoa na mtangazaji wa Cool FM ya Nigeria. Wawili hawa walitumia muda wa hapo ndani kupiga picha za pamoja huku kila mmoja kuoneka akiwa kwenye hali ya kufurahia kila kinachoendele hapo.

Dalili zilizoonyesha kwamba bifu lao linakaribia kuisha au limeshaisha nyuma ya pazia ni pale D Banj alipomuita Don Jazzy kwenye stage waimbe pamoja. Kitu ambacho watu wengi walijua kisingewezekana, lakini Don Jazzy aliungana na D Banj na wakaimba pamoja ngoma zao tatu kali na kuonekana wakiwa kwenye muonekano na hali kama ya zamani enzi za ushkaji

Mitandao mingi ya Nigeria imeandika kwamba kuna uwezekano kwamba Don Jazzy na D Banj wameshamaliza tofauti zao.

No comments