Skylight Band inakukaribisha usiku wa leo Thai Village kwa burudani ya kipekee kabisa!
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba pamoja na Sam Mapenzi.
Aneth Kushaba sambamba na Digna Mbepera wakiwapa raha mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya ukumbi wa maraha wa Thai Village Masaki jijini Dar.
Kifaa kipya cha Skylight Band Bela Kombo akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wa Thai Village Ijumaa iliyopita.
Kutoka kushoto Bela Kombo, Hashim Donode na Digna Mbepera wakiporomosha burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village.
Binti mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera kwenye hisia kali za muziki wa Live kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
Burudani ikiendelea.
Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na muziki safi kabisa wa ladha na vionjo vya kila aina ikiwemo Reggae, Kwaito, Naija Flava, R&B, Zouk na zingine kibao bila kusahau sebene pale kati Joniko Flower anahusika sana sambamba na Sony Masamba njoo ufunge mwezi Oktoba na Skylight Band usiku wa leo.
Anaitwa Sony Masamba akifanya yake jukwaani huku Sam Mapenzi na Joniko Flower wakipiga back vocal.
Oya shake body….Oya move body….Make you ring alarm o….Oya shake body….si mwingine ni Sam Mapenzi na Naija Flava njoo leo umshuhudie kwa macho yako…Skylight Band ndio kila kitu huna haja ya kwenda disco unapata kila kitu hapa hapa…!
Aaaah ni full raha wake kwa waume wakionekana kukunwa na uimbaji wa Sam Mapenzi mzee wa Naija Flava, unakosaje uhondo ndugu….Njoo tujumuike leo pamoja ndani ya Thai Village.
Umati wa mashabiki wa Skylight Band wakiyarudi mangoma ya ukweli yaliyoenda shule, tukutane pale kati kuanzia saa tatu usiku.
Mpiga drum wa Skylight Band Baraka akifanya yake kuhakikisha mashabiki wanapata ladha nzuri ya ala hizo za muziki huku pale pembeni Amos Kinanda naye akisababisha.
Na hivi basi ndivyo wanavyochizika mashabiki wa Skylight Band kwa shangwe za aina yake mwenye kigelegele haya…mwenye mluzi haya….ni furaha si kingine.
Mkongwe wa muziki Joniko Flower akiwasebenesha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku waimbaji wenzake wakimpa sapoti.
Sam Mapenzi;……Kuna Watu Hatari, Wenye Mapenzi Zenye Siri Kali,…Letu Nalo Lina Jua Kali, Penzi Letu Serikali,….Wajua Nakupenda, Malaika…..Aneth Kushaba;…..I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)….I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,….(Aiyayaaaaa)…Hizi zote utazipata Skylight Band si kwingine bonge la colabo.
Nyomi la mashabiki wa ukweli wa Skylight Band likiwa limefurika Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.
Supermodel Neema Mbuya akionyesha upendo kwa mpiga picha na busu bashasha….Santeeee!
We are twin sisters……!
Blogger King Kif (kushoto) akiwa na wadau wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
Meneja Maneno na King Kif wakimezea mate kuku choma ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
No comments
Post a Comment