HEBU FIKIRIA KUWA UMEDHIBITISHA KWAMBA MWENZAKO SIO MWAMINIFU, YAANI AMETOKA AU ANATOKA NJE YA NDOA, UTAFANYAJE? JE, UTAONDOKA, UTALIPA KISASI NA WEWE, AU UTACHUKUA HATUA GANI?...
Kuna Mambo Ambayo Ukiona Kwamba Yamejitokeza, Baada Ya Fumanizi, Unapaswa Kujua Nafasi Yako Kwenye Uhusiano Wako. Kutokea Hapo Ndipo Unapoweza Kuamua Kama Uondoke Au Hapana.
Kwanza, Hebu Jikague, Je, Umevunjika Moyo Kupita Kiasi? Unadhani Itakuwa Bora Kuvumilia? Unadhani Kumvaa Na Kumwambia Umechoka Na Unataka Kuondoka Itakuwa Ni Kujiongezea Mfadhaiko Zaidi?
Pili, Unadhani Utaendelea Kubaki Katika Ndoa Kwa Sababu Za Kidini? Unataka Kufanya Kitu Kilicho Sahihi Daima? Uko Tayari Kuendelea Kudhalilika Na Kuwa Hatarini Kwa Sababu Ya Imani Yako Ya Kukukataza Kuvunja Ndoa? Je Ni Kwa Imani Yako Au Wasiwasi Wako Umelazimika Kubaki? Nijuavyo Mimi, Kosa La Kutoka Nje Halitetewi Na Dini Yoyote Linapokuja Swala La Kuvunja Ndoa.
Tatu, Unadhani Unalazimika Kubaki Kwa Usalama Wa Watoto? Unadhani Ni Wewe Pekee Unawajali Watoto Na Mwenzio Hawajali? Inawezekana Na Mzazi Mwenzio Pia Ni Mpenda Watoto? Unadhani Kuachana Kutawaletea Watoto Matatizo Zaidi? Una Wasiwasi Na Maisha Ya Watoto Kama Utaamua Kuondoka? Kumbuka Kuishi Kwenye Vurugu Za Ndoa Huwavuruga Watoto Kuliko Watoto Kuishi Na Baba Au Mama Wa Kambo Mwenye Upendo.
Nne, Unadhani Hakuna Uwezekano Kabisa Katika Ndoa Hii? Umekwama? Umenata Kama Ulimbona Huwezi Kuondoka? Unaweza Kufikia Muafaka Kwamba Umejitahidi Kwa Uwezo Wako Wote Kumrekebisha Mwenzio Lakini Wapi. Hivyo Umeamua Kuishi Hivyo Hivyo?
Tano, Unadhani Huwezi Kuondoka? Kuna Kitu Unachodhani Kinakuletea Ugumu Wa Kuanza Safari? Kuanza Maisha Mapya? Huna Uwezo Wa Kujiamulia? Kumbuka Kwamba, Huenda Ni Mazoea Tu Yanayokuzuia Au Utegemezi Wa Kipato. Lakini, Kila Binadamu Ameletwa Duniani Ili Asimame Kama Yeye, Na Siyo Kama Kipande Cha Mwenzake.
Sita, Unataka Kumlinda? Kuna Kitu Kibaya Unachodhani Kinaweza Kutokea Kama Utaamua Kuondoka? Ataweza Kuishi Peke Yake? Kama Utaondoka Unadhani Itakuwa Ni Njia Ya Kumpeleka Shimoni Zaidi? Umeamua Kubaki Ukijua Kwamba Baada Ya Muda Tatizo Lenu Linaweza Kutatuliwa? Inawezekana Likatatuliwa, Lakini Inawezekana Wewe Ni Mtu Wa Kuumia Kwa Sababu Ya Wengine Bila Sababu.
Saba, Unaendelea Kuishi Naye Kwa Sababu Kuna Hatari Kumwambia Unataka Kuondoka? Unadhani Atalipuka Kwa Hasira Utakapomwambia Unataka Kuondoka? Una Wasiwasi Kwamba Una Haki Ya Kuamua Kuhusu Maisha Yako Na Kuna Sheria Zinazokulinda.
Je, Hujafikiria Namna Ya Kuanza Maisha Mapya? Hii Ni Tofauti Na Hofu Ya Kuanza Maisha Mapya. Labda Maisha Yako, Yake Na Ya Watoto Yameambatanishwa Kupita Kiasi, Hivyo Inakuwia Vigumu Kujinasua? Pia Kuambatanishwa Huku Labda Ndiko Kunakokufanya Hata Usiwe Na Chembe Ya Wazo La Kutaka Kuondoka? Umewahi Kufikiria Kuhusu Utashi Wako, Ujuzi Wako, Ndoto Zako, Matumaini Yako Na Mustakabali Wa Maisha Yako Bila Yeye, Au Bila Watoto?
Chukua Muda Wa Kutosha Kufikiri Kwa Makini Na Uyajibu Maswali Hayo Yote Ukishayajibu Utakuta Unatoa Uamuzi Sahihi Utakaokupeleka Kwenye Maisha Uyatakayo. Kumbuka, Kila Binadamu Hukosea Na Kusamehe Kwa Aliyekosewa. Lakini Kusamehe Hakuna Maana Ya Kuendelea Kuumia Au Kuumizwa Na uliyemsamehe........unaweza ukasamehe huku ukiendelea na maisha yako na kutimiza ndoto zako na malengo yako maishani.
No comments
Post a Comment