LEO
tunatimiza miaka kumi toka kifo cha mwanamuziki mahiri Freddy Supreme
au maarufu kama Ndala Kasheba. Freddy alianza kufundishwa gitaa na baba
yake wakati akiwa na umri wa miaka 12. Baba yake alijua kupiga gitaa
japo hakufanya kazi ya uanamuziki, alikuwa akipiga gitaa nyumbani baada
ya saa za kazi. Moja ya bendi maarufu ambazo zilimtambulisha sana Fredd
ilikuwa Orchestra Fauvette, Freddy alieleza kuwa bendi ya Orchestra
Fauvette ilianza tarehe 7 mwezi wa sita mwaka 1964 katika jiji la
Lubumbashi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Jina hilo Fauvette kwa
kiswahili ni Chiriku, bendi ilikuwa na muimbaji ambaye waliamini alikuwa
anaimba kama chiriku na hivyo kuipa bendi hiyo jina hilo. Vyombo vyao
vya muziki walinunua Ujerumani kupitia duka la muziki la Dar es salaam
Music House (duka lipo mpaka leo). Vyombo vilikuwa vya aina ya Hofner,
jina lililoheshimika sana kwa wanamuziki wakati huo.
Kaburi la Kasheba- Kinondoni
Kati
ya nyimbo ambazo zilipigwa katika kipindi hicho ni Camarade ya nzela,
ambayo Freddy alieleza ni wimbo uliokuwa ukizungumzia rafiki wa kukutana
nae barabarani au njiani, ambaye roho yake huwa kama sanduku la nguo,
ambalo ndani yake huwezi kujua kuna nini. Pia ulipigwa wimbo Jacqueline
ambao ulitungwa na mwenyewe Freddy ambao alieleza alikuwa alimtungia
mpenzi wake aliyempenda Jacqueline. Wimbo mwingine uliopigwa katika
kipindi hicho ni Nono na Kalemie, wimbo huu ulitunguiwa binti aliyeitwa
Nono mkazi wa Kalemie ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa bendi ya Fauvette.
Fauvette ilifika Dar na kuwa inapiga katika ukumbi wa White House
Ubungo, lakini kwa miaka hiyo Ubungo ilikuwa mbali sana na mji, na
kulikuwa na ajali nyingi zikiwapata wapenzi wa bendi katika usafiri wa
kutoka kwenye muziki, hivyo bendi ikaamua kuhamia ukumbi wa Mikumi Tours
ambapo walikuwa wakipiga Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Fauvette
walikuwa na ndoto ya kuwa bendi bora Afrika. Hawakufikia huko lakini
waliweza kuweka alama kubwa katika historia ya muziki wa Afrika
mashariki na Kati
Kasheba
aliweza kuimarisha jina lake zaidi alipolifanya maarufu gitaa la nyuzi
kumi na mbili, mwenyewe akiliita nyuzi dazani, hasa alipoanza kulipiga
kwa mtindo wa Dukuduku akiwa Safari Sound Orchestra. Pamoja na bendi
hizo Kasheba pia alipitia Safari Nkoy, Zaita Muzika, Kasheba group, pia
alipita Maquis, na kwa wiki chache alipitia Tancut Almasi.
Kasheba alifariki 22 Oktoba 2004 akiwa na miaka 58.
.
MJUE MWANAMUZIKI NA MPIGA GITA MAARUFU TANZANIA, NA HII NI HISTORIA YAKE HADI MAUTI YALIPO MKUBWA..
Reviewed by Unknown
on
11/09/2014
Rating: 5
No comments
Post a Comment