CIA yatetea mbinu zake za mahojiano
Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, John Brennan, kwa mara nyingine ametetea matumizi ya mbinu za kikatili wakati wa kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi baada ya shambulio la Septemba 11 nchini Marekani.
Brennan amekiri kuwa baadhi ya mbinu zilizotumika zilikuwa za kuchukiza.
Lakini amesisitiza kuwa baadhi ya wafungwa ambao walipitia mbinu hizi, ambazo zilikuwa ni pamoja na kuwazamisha kwenye maji, kufadhaisha na kuwanyima usingizi zilisaidia kuokoa maisha ya Wamarekani na zilisaidia kumpata Osama bin Laden.
Amesema alikuwa akijibu ripoti ya Kamati ya Upelelezi ya Baraza la Senate la Marekani, ripoti ambayo imekosoa vikali mbinu za mahojiano za CIA, ambazo zinasemekena zimekuwa za mateso kwa watuhumiwa
Baadhi ya vitendo vinavyodaiwa kufanywa na CIA ni pamoja na kuwamwagia maji watuhumiwa,kuwanyima usingizi na hatua nyingine ambazo ni kinyume na haki za binadamu.
No comments
Post a Comment