RIDHIWANI AKIKABIDHIWA ZANA ZA JADI
Wazee wa kijiji cha Msoga,katika kata ya Msoga ,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ,wamemkabidhi zana za jadi mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ikiwa ni moja ya ishara ya kumpokea kijijini hapo rasmi..
Wazee hao walifanya shughuli hiyo mapema juzi na kumtaka mbunge huyo kuendelea umoja na mshikamano nadani ya jimbo hilo.
Nae Ridhiwani Kikwete akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zana hizo amewashukuru wazee hao na kuahidi kutekeleza masuala ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kutoka katika hatua iliyopo sasa.
Aidha Ridhiwani amesema suala la mila na desturi linatakiwa lidumishwe pasipo kulipa kisogo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae .
No comments
Post a Comment