Kajala kugharamia ndoa ya Wolper
Kajala Masanja (kushoto) ameahidi kugharamia kila kitu katika harusi ya rafiki yake Jackline Wolper na Manaiki Sanga
Mrembo anayefanya vizuri katika soko la filamu nchini, Kajala Masanja, amejinadi atagharamia kila kitu katika harusi ya rafiki yake Jackline Wolper na Manaiki Sanga.
Alimwambia Mwandishi Wetu kuwa Wolper na Manaiki, wametangaza rasmi nia ya kutaka kuoana.
“Siyo kama naongea ili niandikwe kwenye vyombo vya habari, ukweli ndiyo huo.
“Mimi nitagharamia kila kitu katika harusi yao, hii ni kutokana na ukaribu wangu na wao, Sanga alikuwa na ndoto za siku nyingi kumuoa Wolper, nitafurahi hilo likitimia,”alisema.
No comments
Post a Comment