
Mwishoni mwa msimu huu kiungo wa
Liverpool Steven Gerrard atakuwa akiiaga timu yake hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 17 na kuhamia katika klabu mpya ya
Galaxy ya Marekani ambapo ametengewa dau kubwa kwa ajili ya kwenda kuitumikia.

Galaxy imemwandali kiungo huyo hatari na kipenzi cha mashabiki wengi maisha mazuri akiwa na timu hiyo ikiwa ni pamoja na mshahara mzuri na jumba la kifahari ambalo unaambiwa thamani yake ni pauni milioni 16.8.

Steven Gerrard akiwa na familia yake
Gerrard atahama Liverpool akiwa tayari amedumu kwa miaka 17 sambamba na mkewe Alex na mabinti zake watatu katika jumba hilo lililopo kwenye ufukwe waMalibu Magharibi mwa Marekani.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote
No comments
Post a Comment