Header Ads

Breaking News

Ghana yatangaza siku tata za maombolezo ya kitaiafa

Zaidi ya watu mia moja wamepoteza maisha kutokana na ajali ya moto kwenye kituo cha mafuta mjini Accra, Ghana, Juni 3 mwaka 2015.







Nchini Ghana, zaidi ya watu mia moja wamepoteza maisha katika ajali ya moto iliyotokea katika kituo cha mafuta mjini Accra. Watu hao walikuwa wakikimbia mvua kubwa na walikimbia karibu na pampu za mafuta kwa ajili ya kujihifadhi. Serikali ya Ghana Siku tatu imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Miili ya watu imeendelea kutolewa kutoka eneo la tukio na kuwekwa katika malori. Serikali ya Ghana bado inajaribu kupata idadi kamili ya watu waliokufa au kuathirika kutokana na ajali hiyo. Wengi wa waliokufa walijihifadhi katika kituo cha petroli kukwepa mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ambayo imesababisha mafuriko katika sehemu kubwa ya mji wa Accra.
Rais wa Ghana John Dramani Mahama ametangaza Alhamisi wiki hii siku tatu za maombolezo ya kitaifa ya siku tatu baada ya kutokea kwa mlipuko wa kituo cha mafuta jijini Accra uliosababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja. Amesema shughuli za uokozi zitaendelea hadi mwishoni mwa juma hili, na siku ya Jumatatu ndio maombolezo yataanza.
Wengi wa watu hao walikuwa wamejihifadhi mvua kubwa ziliizokuwa zikinyesha wakati ulitokea mlipuko kwenye kituo hicho na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100 katika eneo la Kwame Nkruma, kunakopatikana kituo hiki cha mafuta.
Inaelezwa kwamba moto huo ulianzia jirani na kituo hicho kabla ya kufikia kwenye mapipa ya mafuta yalioanza kulipuka na kusababisha sio tu asara za watu kupoteza maisha lakini pia mali na vitu vilivyoteketea.
Idadi hiyo ya watu waliopoteza maisha huenda ikaongezeka. Rais Mahama aliezuru katika eneo la tukio ameonekana kuguswa sana na tukio hilo na kutangaza maombolezo ya siku tatu.

No comments