Header Ads

Breaking News

URAIS 2015, UMOJA WA WALIMU WAMUUNGA MKONO LOWASSA.....

  Sufyan Omar's photo.

Umoja wa vuguvugu la mabadiliko ya walimu Tanzania, limesema linamuunga mkono Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, kugombea urais wa awamu ya tano....
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, walimu hao walisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kwa kuwa wanaamini akipata nafasi ya urais atafanya mambo mazuri sana hususani katika sekta ya elimu..
  Sufyan Omar's photo.
 Mwenyekiti wa umoja huo, Ally Umakuli, alisema wanaamini kwamba Lowassa atafanya mambo makubwa akiingia madarakani kwa kuwa hata kipindi akiwa Waziri Mkuu alifanya mambo makubwa ikiwemo kujenga shule za sekondari kila kata na hivyo kuimarisha ajira kwa walimu...
Sababu ya pili, alisema kati ya waliojitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo mpaka sasa, hakuna aliyejitokeza na kuonyesha vizuri namna ya kuipa kipaumbele sekta ya elimu na uhakika wa maslahi kwa walimu kama alivyoeleza Lowassa....
Tatu, walisema Lowassa ni mtia nia pekee mpaka sasa ndiye anaonyesha kuwa mshirika katika matatizo mbalimbali ya kutatua changamoto za walimu na elimu, na kwamba mwaka 2013 alishiriki katika harambee ya madawati katika shule za sekondari za tarafa ya Mbagala na kufanikisha kupatikana madawati 800 na zaidi, pamoja na kushiriki kutunisha SACCOSS ya Mkoa wa Kilimanjaro ambayo zaidi ya billioni moja zilipatikana...
Pia walisema, Lowassa alisimamia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na pia wanamwamini kwamba atasaidia katika sekta ya elimu kuliko mgombea yeyote yule, ana mapenzi ya dhati kwa walimu.....
Walisema wanamwamini kwamba akiwa rais posho za walimu, nyumba, vifaa vya kufundishia, malipo ya madeni pamoja na ongezeko la mishahara litashughulikiwa ipasavyo.... Pia Ndg Ally alisema wanaamini hata maduka maalum ya walimu yataanzishwa kama ilivyo kwa wanajeshi na askari polisi....
"Matatizo ya walimu nchini yapo kila kukicha hakuna suluhisho badala yake ni maneno tu, walimu tumedhamiria kwa dhati kwamba sauti ya rais ambayo leo hii tumeitangaza ni sahihi na itatusaidia, tumefanya ili ajue kabisa kwamba tuko nyuma yake katika kufikia lengo lake ili atutatulie kero, matatizo na changamoto mbalimbali za walimu na tumeamua kufanya hivi wakati tunaelekea kumpata rais mpya tukijua kwamba tutatumia haki ya kupiga kura ya kimakubaliano ya maslahi yetu walimu wote" alisema (NIPASHE)... 4.06.2015

No comments