WATU WALIOKUFA KWA MOTO KATIKA JIJI LA ACCRA WAFIKIA 150
Idadi ya watu waliokufa katika tukio la moto kwenye kituo cha mafuta katika Jiji la Accra nchini Ghana imefikia watu 150.
Moto huo uliotokea jumatano umetokea wakati watu wakikabiliana na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili, iliyowaacha watu wengi bila ya makazi, wala umeme.
Mafuriko yamekuwa yakiathiri jitihada za kuokoa watu, na huenda ndio yaliyochangia kutokea mlipuko wa moto huo.
You might also like:
No comments
Post a Comment