Header Ads

Breaking News

Tarime: John Heche(Mb), Akamatwa na Polisi Kwa Tuhuma za Kuhamasisha Bangi na Uvamizi wa Mgodi

Tarime: John Heche(Mb), Akamatwa na Polisi Kwa Tuhuma za Kuhamasisha Bangi na Uvamizi wa Mgodi

Polisi wamefika Nyumbani kwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche,
sasa Hivi wa naomba kuchukua simu zake zote na wanamueleze Kuwa anatuhumiwa kwa kuchochea wananchi kuvamia Mgodi wa ACIACIA. Kosa la Pili analotuhumiwa nalo ni Kuhamasisha Kilimo cha bangi. Alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara Silali, aliwaambia wananchi kwamba atapeleka Hoja binafsi bungeni ili bangi iwe zao la Biashara. Kwa sasa yupo chini ya Ulinzi.

=> Polisi Wamechukua simu moja na Ipad ila kakataa kuwapa Password.

=> Vilevile Polisi Wamemtaka Esther Matiko Mbunge wa CHADEMA Tarime Mjini, Kujisalimisha Polisi aunganishwe kwenye kesi ya Heche kwani na yeye alikuwepo kwenye Mkutano wa Silali.


UPDATES;1630hrs

Hatimaye Mbunge John Heche aachiwa kwa dhamana. "Wamemwachia Heche ila wamechukua simu zake zote na kumtaka afike polisi Jumatatu kwa mahojiano. Leo amekataa kuchukuliwa maelezo yoyote kwa kuwa hakuwa amekwenda Polisi kwa mambo hayo bali kushughulikia kukamatwa kwa Katibu wake, hivyo amejidhamini na kuondoka ila simu zimebaki Polisi"


Source:Jamii Forums

No comments