Header Ads

Breaking News

AHUKUMIWA MIAKA SITA JELA KWA KUMCHOMA MTOTOWAKE (NIGERIA)

Ni siku kadhaa tu zimepita toka mwanamke mmoja mkoani Mbeya kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumnyanyasa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu ambae ni wa dada yake ambapo alimchoma na kusababisha akatwe mkono pamoja na kumlazimisha kula choo.
Huko Nigeria nako stori inayofanana na hii imeingia kwenye headlines, ni binti wa miaka 18 ambae amehukumiwa jela miaka 6 baada ya kupatikana na hatia ya kumchoma moto mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka miwili ambae aliokolewa na msamaria mwema ambae anaishi eneo hilo la Osogbo.
Sababu zilizotolewa na binti huyu za kumchoma mwanae, ni maisha magumu aliyonayo hivyo alilazimika kufanya hivyo ili asafiri mpaka kwenye mji wa Lagos kutafuta ajira na asingeweza kutafuta kazi wakati bado anaendelea kumlea mtoto huyo wa miaka miwili.
Amewalaumu pia wazazi wake na baba wa mtoto ambao kwa pamoja walimtelekeza hivyo akawa hapati msaada wowote kutoka kwa yeyote..

No comments