UNYAMA ALIOFANYIWA MWAFUNZI (MBEYA)
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya Daniel Godluck Mwakyusa (31) aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].
Indaiwa Marehemu akiwa na wenzake wanne walikuwa katika starehe ya kawaida kama ilivyokuwa kwa wengine walioipa umuhimu siku hiyo.Wakiendelea na starehe yao pale Univesal Pub Uyole polisi waliokuwa doria walikuta vijana hao wakipata vinywaji ndipo waliwatuhumu kuwa ni majambazi ambapo PC Maduhu alimpiga marehemu risasi mbili kwa kutumia bunduki aina ya [SMG].
Inaelezwa kuwapia marehemu aliporwa fedha taslimu kiasi cha shilingi laki tatu pamoja na simu ya mkononiambayo haikufahamika mara moja aina na thamani yake
Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu huyo Bwana Pastory Mwakyusa amesema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho kilichotokea kwani mwanawe hakuwa na tabia ya wizi au ujambazi hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kueleza sababu ya kumuua mtoto wake.
Jeshi la Polisi lilitoa usafiri wa gari lenye nambari za usajili T 138 AFK aina ya Coster kwa ajili ya kusafirisha Mwili wa marehemu kwenda katika wilaya ya Kyela kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari kuthibitisha kuwa marehemu ameuwawa kwa risasi.
Swali ni je tangu lini jambazi,ama mwizi akagharamiwa na jeshi la polisi namna hiyo?
No comments
Post a Comment