SERA ZA CHAMA
Kauli mbiu ni sera au Ilani ya chama?
KUNA usemi usemao kuwa
utasoma sana, utasahau sana na utajua machache (the more you learn, the more
you forget and less yo know)
Katika harakati za
kulaza chama cha Demokrasia, CHADEMA kumejikita katika kusaka wafuasi na
viongozi kutoka katika vyuo vikuu. Wenyewe wakiwa na imani kubwa kwamba wasomi
wataweza kukivusha chama vizuri hatimaye kushika dola.
Kwa bahati mbaya CHADEMA wamekosa ufahamu kuwa
wasomi ni makarani kwa kiasi kikubwa. Wasomi sio wanasiasa bali ni watendaji
wazuri wa ofisini. Na kauli hii inathibitisha na mwenendo mzima wa kisiasa wa
CHADEMA.
Pamoja na kuwa
wamepata mafanikio makubwa kukonga nyoyo za vijana wa vyuo vikuu, lakini mikiki
mikiki ya kisiasa bado inawapa shida kubwa.
Siasa inahitaji watu
makini na wenye vichwa vilivyotulia sio watu wa kucharuka haraka. Na kwa msingi
huo basi uongozi mzima wa CHADEMA umeshindwa kuweka hadharani sera yao hasa ni
ipi na ilani yao inasimama kitu gani, badala yake wanachukua muda mwingi
kuzungumzia ufisadi. Na kuchukulia ufisadi kuwa sera halisi ya chama.
Katika kipindi hicho
hicho cha matengenezo ya ufisadi, CHADEMA watakaouchukua katika kudhibiti
ufisadi. Kwa hiyo chama hiki walipaswa kumueleza umati wa Watanzania mbinu
zilizo wazi ambazo wao katika utekelezaji wao watafanikiwa kuzuia ufisadi,
vinginevyo watakuwa wababaishaji tu ambao siasa zao zimejaa ulaghai.
Nasema ulaghai kwa
sababu pamoja na kuwa chama kimesheheni watu wenye digrii moja hadi wengine
wamesahau idadi ya digrii walizosomea, wameshindwa kutofautisha kauli mbiu na
ilani ya chama ambayo hufafanuliwa katika sera.
Kauli mbinu zimejaa mpaka
hawajui ipi itumike kwa kipindi gani. Walikuwa na operesheni sangara hatujakaa
vizuri tukaambiwa maisha magumu mara ukaibuka ufisadi tena maandamano mpaka
kieleweke.
Hali haijatulia M4C.
mikakati yote hii haiendi mbali kwa sababu haina Baraka katika sera na ilani ya
chama.
Leo ukiwauliza wabunge
wao ni kwa kiasi gani wametafsiri sera rasmi ya chama chao sina uhakika iwapo
watatoa jawabu moja lenye kufanana kwa mujibu wa sera ya CHADEMA.
Au katika majimbo
walikochaguliwa ni kwa kiasi gani wabunge wametekeleza sera za chama chao
kulingana na ilani ya chama chao.
Wabunge na viongozi wa
CHADEMA sio wa kweli na pia sio waaminifu hata kidogo kwa sababu katika
mahubiri yao mengi wakiwa peke yao na wafuasi wao, huwadanganya na kuwapotosha
wafuasi wao eti serikali haijafanya lolote la maana kwa miaka yote hamsini
tangu ilipoanza kutawala.
Lakini viongozi hao
hao wanapokutana na kiongozi mkuu wa serikali Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete hupiga
makofi mpaka idadi yake huwapotea. Baada ya kushangilia kwa makofi na
vigelegele, hufuatia mapambio ya kumsifu Mhe. Rais wetu Kikwete kuwa anastahili
pongezi na kuungwa mkono katika juhudi zake za kujenga uchumi wan chi kwa
kuimarisha mawasiliano kila mahali.
Mambo mengine ya
mapambio nimeyafahamu. Mfano hai ni pale Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete
alipokuwa ziarani Rombo na kule Hai. Mbunge wa Rombo Mhe. Selasini (CHADEMA)
alimwaga pongezi lukuki kwa Rais.
Baadaye kule Hai kwa
Mhe. Mbowe Waziri Mkuu kivuli na Mwenyekiti wa CHADEMA yeye tena katika
mapambio yake hayasemeki na haikutarajiwa maneno yale yatoke kinywani mwa
Mbowe. Lakini ndio hivyo ameyasema na watu tumeyasikia.
Swali la kujiuliza
kumbe uongozi wa CHADEMA mnajua mazuri ya serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete
kwanini hawawaelimishi wafuasi wao hali halisi ya kisiasa kwa upande wa
serikali na wao CHADEMA wanatofautiana nini au kwa upande upi na serikali?
Haya hayasemeki kumbe
siasa za CHADEMA ni za woga. Wakiwa peke yao wamesema mengine wakikutana na hao
wenye serikali yao wanasifu mengi.
Kimsingi uongozi wa
chama hiki wote wana ndimi mbili. Hazijulikana ni ulimi upi husema lililo la
kweli na ulimi upi na upande gani husema yaliyo na uongo.
Babu yangu alinisimulia
hadithi wakati huo wa kukaa na kucheka na babu kwamba nyani akiwa porini na
wanyama wenziwe basi nyani husimama kwa miguu miwili na kuwakoga wanyama
wenzake kwamba yeye ni binadamu.
Lakini, atakapo tokea
binadamu wa kweli nyani hurudia unyama wake na kutembea kwa miguu na mikono.
Kwa kufanya hivyo wanyama wenzake humdhihaki kuwa nyani sio lolote wala
chochote kumbe mwoga kuliko kunguru.
Hivyo, uogozi wa
CHADEMA mbele ya viongozi wa serikali na CCM huwa wadogo wakiamini na kutii
kama wafanyavyo raia wengine na kuthibitisha kuwa wao ni viongozi bandia.
Rais Kikwete alisema
kuwa yeye ndio Rais wa Tanzania na nao CHADEMA hawana Rais mwingeni na hawana
kwa kwenda isipokuwa kwake. Kweli leo CHADEMA wale wale waliosema mpaka
kieleweke na wataandamana bila ya kikomo, sasa wanamuimbia mapambio Rais
Kikwete.
Kwanini CHADEMA
wanashindwa kutunga na kujenga hoja kupitia sera za chama chao. Kwa sababu
wamejaza ‘madeski ofisa’ sio wanasiasa hivyo hoja za kisiasa CHADEMA zinakosa
majibu yaliyo sahihi.
Ukosefu wa sera kwa
chama kupelekea mapungufu yanayopatikana. Kwa kukosa sera CHADEMA wanakosa
majibu kwa serikali juu ya matatizo mbalimbali yanayojitokeza hapa nchini.
Ukifuatilia kwa karibu
hoja za CHADEMA zote zimejaa lawama na malalamiko bila ya kutoa jawabu mbadala
la mtatuzi wa matatizo yanayojitokeza. Wamejikita kwenye itikadi za uliberali
lakini kilichowazi ni kwamba huko wamefuata masilahi tu.
Wao CHADEMA walijua
fika kwamba ukijichanganya katika makundi utafanikiwa kupata misaada kutoka nje
na kufanikisha mambo yako. Lakini, kinyume cha masilahi binafsi kutoka katika
jumuiya waliberali hatujawasikia CHADEMA wakiueleza umma wa Watanzania
uliberali unataka nini kijamii, kisiasa, kiuchumi na utamaduni.
Nina imani kubwa
kabisa hata Dk. Slaa, Marando, Tundu Lissu, Prof. Safari, Prof. Baregu
hawajaota iwapo wao wanawajibika kuwafundisha uliberali wana CHADEMA.
Hivi Erasto Tumbo kule
Meatu au Baradi wanajua madhara ya uliberali? Je Bw. Singo kule Bomba mbili au
Mfaranyeki wanajua sera ya uliberali au Bw. Mnyika Manzese Sinza na Ubungo
wanayo taarifa juu ya sera ya uliberali?
Rasilimali maji
ugawanyo wake ukoje kiliberali. Sasa utaona hakuna hata kiongozi mmoja ndani ya
CHADEMA hata Mwenyekiti wao mwenye dhamana ya kuisimamia sera ilani na katiba
anaeizungumzia sera ya uliberali.
Sina uhakika iwapo
itikadi ya uliberali imo au imeingizwa katika katiba ya CHADEMA na kama
imeingiziwa ni kiasi gani cha uelewa wa wana CHADEMA juu ya sera itikadi ya
chama chao.
Vinginevyo ufisadi M4C
kugeuzwa sera itikadi ilani itakuwa wamewatapeli wazungu wanaotoa nguvu zoa kwa
kuamini zinafanya kazi kumbe huku zinakwenda kushoto kulia.
CHADEMA semeni sera
yenu itambulike ili ikosolewe ikibidi. Kauli mbiu sio sera. Jibuni hoja za
kisiasa kwa sera za chama chenu ili mwelekeo na matarajio yenu yawe wazi.
Kumbukeni usemi njia
ya mwongo ni fupi kwa kukosa sera hata mkibahatisha kuingia Ikulu mtaingia
mlango wa mbele mtatokea mlango wa nyuma papo hapo.
NA ROBERT AZGR:
No comments
Post a Comment