MAREKANI YATOA ONYO KALI KWA ZIARA YA RAIS OBAMA TANZANIA.

Dar
es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa
kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili
nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula
ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya
bomba.
itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine
haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania
kwaniSource: www.maishayakwetu.blogspot.com
utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari
za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za
Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao
wanavyoitathmini.
Rais
Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo
vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo
haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya
akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi
huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.
Kwa
mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori
matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye
vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe
wake watafikia.
Kwa
mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi
hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious
ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini,
jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote
itakayotokea
.
Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu
kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo,
iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa
gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za
Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini
safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari
Kwa
mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata
nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia
kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.
“Kutokana
na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa
kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa
kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa
kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.
Deet
ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na
kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu
miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.
ATM
nazo noma
Pia
watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia
mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna
tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu
zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia
teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia
siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama
wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,”
ilitahadharisha taarifa hiyo.
No comments
Post a Comment