Header Ads

Breaking News

HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA LIONEL MESSI JUU YA MASHTAKA YA KUKWEPA KULIPA KODI





Mshambuliaji nyota wa ki-argentina Lionel Messi ameitwa mahakamani tarehe 17 ya September kwenda kujibu shitaka la kukwepam kodi nchini Hispania

Messi 25 mchezaji bora wa dunia mara nne pamoja na baba yake inasemekana kukwepa kodi kwa kuuza nembo yake katika makampuni ya nje ya Hispania kinyume cha sheria na inatajwa kiasi cha euro £3.4m) ingawa wote wamekanusdha shtaka.

Lionel Messi ambaye mshahara wake ndani ya Barcelona unafikia kiasi cha euro 16
million kwa mwaka unamfanya kuwa moja ya wachezaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha pesa duniani pia anamikataba ya mamilioni ya fedha kutokana na mikataba binafsi toka kwa makampuni mbali mbali ya matangazo


Messi na baba yake wanatuhumiwa kukwepa kodi zaidi ya mara tatu kutokana na mauzo ya picha zake nje ya Hispania
Na kama atapatwa na hatia Messi huenda akakumbwa na rungu la kutumikia kifungo jela cha miaka sita na faini kubwa kutokan ana sheria ya kodi ya Hispania.

Lakini mwenyewe Messi kupitia katika ukurasa wake wa Facebook ameandika kwamba kutokana na tuhuma hizo amezikanusha na kusema wao wanafahamu sheria na walifuata utaratibu wote wa kisheria za kodi

Mkurugenzi wa kampuni ya Adidas Herbert Hainer ambaye inadhamini utengenezaji wa viatu anavyovaa mchezaji huyo hakua na subira bali ameweka wazi kwamba ;tutaendelea kufanya kazi na messi kwani ni mchezaji bora na tunajivunia kuwa nae”
 

No comments