MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ''UDSM'' APIGWA RISASI YA TUMBO LEO

Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa
mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na
kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe kompyuta zao na
pochi za fedha.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo,
wanafunzi hao walikubali kuwapa kompyuta hizo na pochi za fedha, na
majambazi kuanza safari yao ya kuondoka bila kuwadhuru.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa bila kupata majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi.

Kwa sasa
mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka
sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka....
No comments
Post a Comment