Lema: Serikali haitambui maji ni biashara
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godlbes Lema (CHADEMA) amesema licha ya
kuwa maji ni uhai, lakini serikali haijatambua kuwa maji ni biashara.
Mbali na hilo, amesema asilimia 70 ya wakazi wa mji wa Arusha
wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama, jambo linalosababisha
wakazi hao kuishi katika mazingira ambayo si salama kutokana na
serikali kushindwa kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa miundombinu
ya maji.
Lema alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la
nyongeza kwa kutaka kujua ni lini serikali itahakikisha inapeleka maji
katika miji mikubwa pamoja na maeneo mbalimbali.
Katika swali la msingi, mbunge wa Bumbwini, Ramadhani Haji Salehe, alitaka kujua tatizo la maji litapatiwa ufumbuzi lini?
Akijibu swali hilo, Naibu wa Wizara ya Maji, Amos Makala, alisema
tatizo la maji nchi bado ni kubwa, lakini serikali inajitahidi
kuhakikisha inalitafutia ufumbuzi na kuwafanya wananchi wote wanapata
majisafi na salama tena ya uhakika.
Alisema mpaka sasa serikali inaendeleza ujenzi wa usanifu wa miradi ya
maji ikiwemo ya kukidhi mahitaji ya lazima kwa sasa na yale yajayo.
No comments
Post a Comment