mwanzo Habari Kitaifa Kitaifa Mbowe: Tabora ni kama vile wamepewa limbwata na CCM
Mbowe alisema hayo jana katika Kijiji cha Choma wilayani Igunga akiwa ziarani katika mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Singida, Morogoro na Dodoma.
Mbowe alisema hayo jana katika Kijiji cha Choma
wilayani Igunga akiwa ziarani katika mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma,
Singida, Morogoro na Dodoma.
Jana, Mbowe akitumia chopa, alifanya mikutano
mitano katika maeneo ya Bukene Mjini, Mwamali katika Wilaya ya Nzega na
maeneo ya Choma, Igulubi na Igunga Mjini.
“Wana-Tabora ni kama vile mmepewa limbwata na CCM,
majimbo yote 10 ya uchaguzi mmewapa CCM lakini mnaendelea kuwa maskini
siku hadi siku, badilikeni,” alisema Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa
Upinzani Bungeni.
Mkoa wa Tabora una majimbo ya Tabora Mjini,
Igunga, Nzega, Bukene, Sikonge, Igalula, Tabora, Tabora Kaskazini,
Urambo Mashariki na Urambo Magharibi ambayo yote yanaongozwa na wabunge
wa CCM.
Alisema wakulima wa Tabora wanaolima mpunga bado
wanakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kwa sababu CCM inakumbatia
matajiri kwa kuwapa vibali vya kuingiza mchele kutoka nje ya nchi.
“Mchele wa nje ukiingizwa nchini unauzwa kwa bei
rahisi wakati mchele wenu unakosa soko na kusababisha hali ngumu, hiyo
ndiyo CCM yenu mnayoipenda,” alisema.
Alisema vyama vya ushirika vilivyopo ambavyo
baadhi vinaongozwa na vigogo wa CCM, vinawadhulumu wakulima wa Mkoa wa
Tabora... “Wakulima wa nchi hii mna msiba mkubwa, msiba huu utakuwa wa
milele kama hamtaungana kuing’oa CCM madarakani.”
Alisema CCM ina wenyewe na kwamba wenyewe hawaishi Igunga, bali Dar es Salaam katika maeneo ya Oystebay, Masaki na Mikocheni.
“Lakini kila wakija CCM mnawapa kura, Mbunge wa
Igunga, Peter Kafumu mlimchagua mkamwacha wa Chadema, je, ametimiza
ahadi zake?” alihoji Mbowe.
Aliwataka wananchi kuacha kuchukiana kwa misingi
ya itikadi zao za vyama na kusema vyama vyote vishirikiane kuangalia
namna vitakavyotokomeza umaskini.
“Nashangaa watu mnachukiana kwa misingi ya vyama
wakati wote maskini, ichukieni CCM iliyoshindwa kubadilisha maisha yenu
kwa muda mrefu,” alisema
No comments
Post a Comment