Header Ads

Breaking News

>LOWASSA- NAWAPONGEZA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA NAPE KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA YA KUKIIMARISHA CHAMA



 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa furaha na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi  yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM,
pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Mhe. Lowassa amewafagilia Kinana na Nape kwa kazi nzuri wanaoifanya ya kuzunguka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama ambapo alimshauri Ndugu Kinana kupunguza kasi wanayokwenda nayo kwani ni kubwa. Pia alisema hakuna katibu wa chama aliyefanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama kama Kinana.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa  kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi  yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizinduw mradi wa umeme vijini (REA) katika kijiji cha Lolkisale,Wilayani Monduli mkoani Arusha.
Pichani kulia,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa (kushoto) wakishiriki kupaka rangi jengo la hospitali ya wilaya,jengo hilo hadi kukamilika linatarajia kutumia kiasi cha fedha shilingi bilioni tisa
 Pichani kulia,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa (kushoto) wakishiriki kuweka vitofali katika jengo la hospitali ya wilaya,jengo hilo hadi kukamilika linatarajia kutumia kiasi cha fedha shilingi bilioni tisa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wakulima wa mpunga wakishiriki kwa pamoja upaliliaji wa shamba la Mpunga,Mto wa Mbu,wilaya Monduli mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa wakitoka kushiriki kupalilia shamba la Mpunga,Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha.

PICHA NA; ZEPHANIA J KAPAYA


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments