Header Ads

Breaking News

STORI KUBWA Ni kweli sarafu ya shilingi mia tano ina madini? Majibu yako kwenye hii video

Meneja BoT
Ilianza kama ishu ya kawaida hivi lakini muda ulivyozidi kwenda ikazidi kuchukua headlines kwenye mitandao ya kijamii kwamba eti kuna watu wananunua sarafu za shilingi mia tano za Tanzania alafu wanatumia madini ya sarafu hiyo kutengeneza vitu kama mikufu hivi !

Sarafu Mia Tano
Nimepitia kwenye channel ya Youtube ya blogger mkubwa Tanzania, Issa Michuzi >>>Michuzi TV na nimekuttana na hii stori nikaona niisogeze hapa kushaare na wewe pia.
Anayehojiwa ni Abdul M. Dollah ambaye ni Meneja Msaidizi wa Huduma za Kibenki Benki Kuu TZ… Majibu yake ni haya kuhusu hiyo ishu; “Huu uvumi tumeusikia wananchui wengi wanakuja na kuulizia habari hiyo, huo ni uvumi tu na sio kweli kwamba kuna madini yoyote katika hii sarafu ya mia tano ambayo yanawez kutengeneza viito vya thamani” >>> Abdul M. Dollah
Wakati tunaizundua hii sarafu mwaka jana tuliwaambia kwamba humu ndani kuna madini yya chuma kwa asilimia 94 na madini ya Nikel asilimia sita tu” >>> Abdul M. Dollah
coin
Video ya Interview hiyo nimekuwekea hapa pia, ukiplay utayapata majibu yote kutoka BoT.




No comments