PETR CECH ATUKANWA NA KUTISHIWA KUUAWA BAADA YA KUJIUNGA NA ARSENAL
Golikipa mpya wa Arsenal, Petr Cech amepokea vitisho vingi vya kuuawa kutoka kwa mashabiki wanaoaminika kuwa wa Chelsea kupitia mtandao wa Twitter baada ya kutua Emirates kwa dau la paundi milioni 10.
Mashabiki hao hawajafurahishwa na maamuzi ya Cech kwenda timu nyingine ya London, licha ya ukweli kwamba ameitumikia timu yao kwa heshimu ndani ya miaka 11 aliyodumu Stamford Bridge.
Watumiaji wengi wa Twitter wanaoaminika kuwa mashabiki wa Chelsea wamemuita Cech ‘Msaliti ‘ na ‘nyoka’, wakati wengine wakisema ‘Cech atakufa kwao, mvaaji wa Helmet ya nyoka”.
Matusi hayo ya mashabiki kwenye mtandao wa Twitter yamekuja baada ya Cech kujiunga na wapinzani wao wakubwa, Arsenal.
No comments
Post a Comment