Header Ads

Breaking News

KIJANA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI BAADA YA KUKUTWA AKIJARIBU KUIBA STOO


Kijana aitwaye Joseph Chacha (17) mkazi wa Majengo Mapya mjini Shinyanga amefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu kuvunja stoo na kuiba mifuko 6 ya unga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema  tukio hilo limetokea Novemba 3,2014 saa moja usiku ambapo kijana huyo alidaiwa kuvunja stoo na kuiba mifuko sita ya unga yenye ujazo wa kilo sita kila mmoja yote ikiwa na thamani ya shilingi 48,000/= mali ya Juma Hassan(40) mfanyabiashara wa Ndembezi mjini Shinyanga.

Kijana huyo alifariki dunia Novemba 4,2014 saa 12 jioni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kwamba chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Wakati huo huo  tukio la pili limetokea Novemba 2,2014 saa 11 jioni katika kijiji cha Zunzuli kata ya Mwenge wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo mtoto wa miezi 7 alikutwa amefariki dunia baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye shimo la maji

Kamanda Kamugisha amesema mtoto huyo alitumbukia kwenye shimbo hilo lenye kina kirefu wakati akicheza na wenzake karibu na nyumba yao.

Kamanda huyo amesema jeshi la polisi mkoani Shinyanga linafanya uchunguzi zaidi juu ya matukio yote matatu na juhudi za kuwabaini na kuwakamata wahusika wa mauaji zinaendelea.

No comments