MCHIMBAJI WA MADINI AUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI
Wachimbaji wadogo wa madini zaidi ya 300 wamemuua kwa kumchoma mwenzao Kulwa Kashinje(22) kitu chenye ncha kali tumboni na sehemu ya makalio yake wakati wakigombania madini huko katika machimbo madogo ya dhahabu ya Kalole kata ya Lunguya wilayani Kahama.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha(pichani) amesema tukio hilo limetokea Novemba 3 mwaka huu saa kumi na nusu jioni.
Akielezea zaidi amesema siku hiyo Kulwa Kashinje(22) mchimbaji wa mdogo wa madini wa Kalole alichomwa kitu chenye ncha kali tumboni upande wa kulia na upande wa kulia wa makalio yake baada ya kutokea vurugu za wachimbaji zaidi ya 300 waliokuwa wakigombea jiwe linalodhaniwa kuwa ni dhahabu katika shamba la Martha Lufunga.
Amesema Kulwa Kashinje alifariki dunia Novemba 4,2014 saa tatu asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
No comments
Post a Comment